Madereva zaidi ya 200 warudi darasani


Agizo la Serikali la kuwataka madereva kurudi darasani ili kuepusha matukio ya ajali za  mara kwa mara imeanza kutekelezwa mkoani Mbeya kufuatia madereva zaidi ya 200 kujiandikisha na kusoma upya sheria ya alama za usalama barabarani. 

Mafunzo hayo yanatolewa kwa muda wa wiki mbili ambapo wahitimu watatakiwa kutembea na vyeti hivyo na vitaanza kutumika baada ya muda ya miezi 6 muda uliotolewa na serikali. 

Mkufunzi wa  mafunzo hayo, Greyson Ngayo na Kamanda wa Polisi Kitengo cha usalama barabarani, Jumanne Mkwama walielezea jinsi mafunzo hayo yalivyoanza. 

"Kabla ya hapo mafunzo yaliyokuwa yakitolewa vyeti vya wahitimu wala havikuwa vikipitia Polisi kusainiwa, lakini sasa hivi ,mafunzo yote yanayotolewa hakuna cheti kinachotolewa hakuna cheti utakachokipata bila kupitia kama Ofisi ya RTO haijakipitia cheti hicho. Na pia nitoe tahadhali huu ndio utaratibu uliopo sasa hivi ukipata cheti ambacho hakijapitia ofisi ya RTO kwenda kuhakikiwa hapo kunakuwa na hualakini, lakini nipende kuwapongeza kwamba vyeti vyenu tunavyo na RTO amevisaini," alisema Ngayo. 

"Sheria na kanuni zote za usalama barabarani mmejifunza lakini kikubwa nataka kuwasisitiza ni hii sheria ya usalama barabarani ya mwaka 73 sio tu inasomwa tu na Mapolisi na wewe kaisome ili hata siku ukipambana na makosa huko umebananizwa unasema aah kumbe walikuwa sawasawa hawakunionea, tunapunguza migongano isiyokuwa na tija ," alisema Kamanda Jumanne.

No comments

Powered by Blogger.