Hizi ndio faida ya juisi ya mbogamboga kwa wenye vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo ni matokeo ya uzalishaji matokeo ya uzalishaji wa tindikali aina ya haidrokroliki asidi nyingi kuliko kiasi ndani ya tumbo ambayo huchangia uharibifu wa utando wa ngozi nyembembe ndani ya utumbo kubwa na tumbo dogo. 

Zipo dalili kadhaa za tatizo hili ambazo huainishwa na wataalam wa afya ambazo ni pamoja na maumivu makali sehemu ya juu ya tumbo ambayo mara nyingi hutokea saa chache kabla ya kula. 

Pia wataalam wanaeleza kuwa miongoni mwa chanzo cha tatizo hilo ni pamoja kula vyakula vilivyokolezwa viungo, kutokuwa na muda maalum wa kula, msongo wa mawazo na mengine kadhaa ambayo si rahisi kuyaainisha yote. 

Sasa hapa naomba kukueleza msomaji wangu kuwa moja ya njia ya kupunguza madhara ya vidonda vya tumbo ni pamoja na kutumia juisi ya mbogamboga. ni vyema kutumia juisi mara kwa mara. 

Unaweza kuandaa juisi ya spinachi, karoti kwa pamoja au juisi ya karoti na matango kwa pamoja kisha ukapata glasi moja kila siku na ukajikuta ukipata ahueni zaidi. 

No comments

Powered by Blogger.