Ifahamu historia ya Jimmy Master (J.PLUS) kwenye Filamu za ngumi


Wengi tunamfahamu kwa jina la J. Plus wengine Jimmy Master lakini jina lake kamili anaitwa Jimmy Mponda. Huyu ni msanii mkubwa sana kwenye Filamu za Action hapa Tanzania yaani filamu za mapigano wengi tumezoea kusema “Movie za ngumi. Jimmy Master ni moja kati ya waanzilishi wa Movie za mapigano hapa Tanzania kifupi ni mkongwe ni miaka 24 sasa toka aanze. Vile vile Jimmy Master  ni mtunzi wa story na pia ni  mwandishi mzuri wa Script mbali na kwamba anauwezo mkubwa wa ku- Direct Movie. 

Kwa wale wenye kumbukumbu tunaweza kukumbuka Jimmy Master alianza kujikita kwenye Movies za mapigano mnamo mwaka 1994 ambapo alifanikiwa kutoa Movie  yake ya kwanza iliyopewa jina la “SHAMBA KUBWA” Movie hiyo ilikuwa nzuri sana na ilipelekea Jimmy Master kuanza kujizolea mashabiki mdogo mdogo katika safari ya uigizaji. Ulipo fika mwaka 1995 Jimmy Master alitoa Movies ya pili ambayo ili pewa jina la “UNGA ADUI”  ulipo fika mwaka 1997 Jimmy Master alitoa Filamu yake ya tatu ambayo ilipewa jina la ‘KIFO HARAMU”. 

Baada ya hapo Jimmy Master alkaa kimya takribani miaka 5 bila kutoa Movie yeyote 2003 akafanikiwa kutoa tena Movies yake ya nne ambayo aliipa jina la “USIA” Kwa namna moja aliendelea kuongeza Mashabiki kutokana na ubora zake ingawa kipindi hicho kulikuwa na changamoto za hapa na pale za vifaa kwa sababu huwezi fananisha na sasa. 

2005 Jimmy Master alijizolea umaarufu mkubwa sana baada ya kutoa Movie yake ya 5 ambayo ilipewa jina la “MISUKOSUKO” ambapo ndani ya Movie hiyo alimshirikisha Sebastian Mwanangulo ambaye naye umaarufu wake ulianzia hapo alipo bamba na jina la “Inspector Seba kumbuka Jina la J.PLUS lilizaliwa kwenye Movie hiyo ya “Misukosuko” ambapo kulitokea na mgawanyiko wa mashakiki yaani kama team za mpira, Mashabiki wa“J.Plus” na Mashabiki wa “Inspector Seba” kutokana na mpambano wao katika muvi hiyo. 

Baada ya Part 1 na Part 2 kuisha Scene za “Seba”team hazikuwepo tena ingawa Misukosuko iliendelea na Part zingine.  MISUKOSUKO ni Movie ambayo ilikuwa na muendelezo mrefu kutokana na kwamba mashabiki waliipenda sana kuliko kawaida.  Hivyo filamu hiyo ilifanikiwa kudumu bila kupoteza ubora na hamu kwa mashabiki toka mwaka 2005 – 2010. Ndipo J.PLUS akaamua kutoa filamu yake nyingine ya Sita ambayo ilipewa jina la “DOUBLE J” huo ulikuwa mwaka 2012. 

Baada ya hapo J.Plus kupitia 'Mzimuni Theatre Arts' ambayo ni yake, 2017 alitoa Movie yake ya 7 ambayo ilipewa jina la ‘The Foundation’ ( Msingi) ambayo kwa upande wake J.plus alimesema “Nategemea hii filamu ya ‘The Foundation’ irudishe heshima ya Muvi za Action hapa Tanzania. Mpaka sasa bado J. Plus anaendelea kusambaza Movie hiyo hapa nchini.

No comments

Powered by Blogger.