Aliyempiga chenga kipa wa Yanga afunguka haya
Mshambuliaji wa timu ya Ndada FC Vitalis Mayanga ambaye jana alimpiga chenga mlinda mlango wa Yanga Beno Kakolanya na kufungwa na bao Nassor Saleh dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza, amesema kuwa bado ana matumaini ya kuendelea kufanya vizuri katika michezo inayofuata.
Mayanga ambaye amefunga mabao 5 mpaka sasa kwenye ligi kuu amesema kuwa ni jambo jema kwa timu yake kupata matokeo kutokana na ushindani uliopo hivyo ili kufikia malengo hayo ni lazima kuongeza juhudi.
"Ushindani kwenye ligi ni mkubwa nasi pia tunahitaji nafasi ya kuweza kupata matokeo mazuri ili kufanikiwa katika hilo ni lazima kuongeza juhudi, sioni tatizo kumtengenezea nafasi mchezaji mwenzangu kwa kuwa wote ni timu moja nitafunga na nitatengeneza nafasi kila inapobidi," alisema.
Ndanda inakuwa ni timu ya pili kumfunga Kakolanya baada ya michezo sita kupita kwani timu ya kwanza ilikuwa ni Mtibwa ambapo Yanga walishinda kwa mabao 2-1 na michezo mingine alifanikiwa kutoka na cllean

Post a Comment