Kagere, Makambo washindwa kuvunja rekodi ya Kibadeni
Mastaa wawili wa Simba na Yanga, Heritier Makambo na Meddie Kagere wameshindwa kuvunja rekodi inayoshikiliwa na Gwiji la Soka nchini, Abdallah Kibadeni 'King Kibadeni' ya kufunga magoli matatu katika michezo hiyo ya watani wa jadi ama Dar es Salaam Derby.
Kibadeni ambaye ni staa wa zamani wa Simba anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee kuwahi kufunga magoli matatu 'hat trick' katika michezo hiyo ya watani rekodi aliyoiweka Julai 19, 1977 katika ushindi wa goli 6-0 ambao Simba iliupata mbele ya Yanga.
Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Uhuru (zamani Taifa) lilishuhudia Kibadeni akiingia kambani mara tatu dakika ya 10, 42 na 89 huku magoli mengine yakiwekwa kimiani na Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika ya 60, 73 na beki wa Yanga Suleiman Sanga akijifunga dakika ya 20.
Katika mchezo wa leo vigogo hao wa Soka nchini walitoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana, na hivyo kuendelea kuiacha rekodi ya Kibadeni ikidumu. Matokeo ya leo yameifanya Yanga kufikisha pointi 13 katika michezo mitano iliyocheza na huku ikiwa ya pili kwenye msimamo wa Ligi nyuma ya Mbao FC yenye alama 14 wakati Simba ambao ni mabingwa watetezi wakiwa na pointi 11 katika michezo sita waliyoshuka dimbani.

Post a Comment