Rais wa UEFA akiri kuwa msimu wa sasa huenda usikamilike
Mkuu wa Shirikisho la kandanda barani Ulaya - UEFA Aleksander Ceferin amesema kuwa msimu wa sasa huenda ukapotea kama hawataweza kuendelea walikoachia ifikapo Juni, ijapokuwa hakufuta uwezekano wa kuuendeleza msimu ujao.
Ceferin ameliambia gazeti la Italia la La Republica kuwa kuna mapendekezo kadhaa yanayoweza kutumika kuukamilisha msimu huu, ambao umesitishwa kote Ulaya kutokana na janga la virusi vya corona. Amesema kuna mpango wa A, B na C.
Kwanza ni kuendelea na msimu katikati ya Mei, Juni au mwishoni mwa Juni, na kama hawatafaulu, basi msimu utakuwa umepotea.
Hata hivyo ameongeza kuwa pia kuna uwezekano wa kuanza tena mwanzoni mwa msimu ujao, na kisha kuuchelewesha msimu unaofuata.
Ceferin amesema kukamilishwa kwa misimu ya ligi za ndani ndilo suala la kipaumbele, hata kama ina maana mechi kuchezwa bila mashabiki

Post a Comment