Uongozi wa Mtibwa Sugar wafunguka kuhusu matokeo mabovu
Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar umewaomba radhi mashabiki wake kutokana na kuwa na matokeo mabaya katika mchezo wao dhidi ya Stand United .
Ofisa habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Stand United ni aina ya matokeo ambayo yanawaumiza hivyo watafanya marekebisho mapema.
"Tuna wachezaji wengi wa ndani, wamelelewa Mtibwa hivyo naamini wakipata uzoefu watarejea katika ubora ambao utatupa matokeo maana ligi msimu huu ni ngumu, mashabiki wasiwe na hofu benchi la ufundi limeanza kufanyia kazi mapungufu," alisema.
Mtibwa Sugar ni miongoni mwa timu ambazo zinashiriki ligi bila ya kuwa na mchezaji wa nje ya nchi na itashiriki mashindano ya kimataifa baada ya kushinda kombe la Shirikisho (FA) mwaka huu.

Post a Comment