Meneja wa klabu ya Yanga afunguka kuhusu Fei toto na Ninja
Mchezaji wa zamani ambaye pia ni meneja wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub Cannavaro ameitaja siri kubwa juu ya mafanikio ya wachezaji mbalimbali wa Yanga ambao wanaotokea Zanzibar tangu wakati wake mpaka sasa.
Hiyo imekuja kufuatia kiungo, Feisal Salum 'Fei toto' kufunga bao safi katika mchezo wa ligi kuu, usiku wa Oktoba 25 dhidi ya KMC ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa taifa.
Akizungumza na www.eatv.tv, Nadir Haroub Cannavaro amesema kuwa Zanzibar kuna vipaji vingi na wachezaji wake wanajitambua ndiyo maana wanafanikiwa wakiwa Yanga, huku akithibitisha kuwa baadhi ya wachezaji hao bado anaishi nao mpaka sasa.
"Ni kweli Fei toto na Shaibu Abdallah 'Ninja' ninaishi nao kwasababu ni watu ambao wanataka kufuata nyayo zangu, hawana tabu na ni wasikivu kwahiyo ninakaa nao kwa uzuri, ndiyo mafanikio hayo unayoyaona sasa", amesema.
Akizungumzia juu ya mchezaji, Said Makapu ambaye aliwahi kuishi naye na baadaye kuondoka na kujitegemea, Cannavaro ameongeza,
"Unajua kuna muda ukifika huwezi kumdhibiti kwasababu kila mchezaji anahitaji kuishi maisha anayoyataka, kuna kipindi nilikuwa nakaa na Said Makapu lakini umefika muda mtu anataka kutengeneza maisha yake kwahiyo inabidi umwache".

Post a Comment