Spika Ndugai 'awapa za uso' vyama vya Upinzani


Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa Rwanda hawana Vyama vya Upinzani vya kupinga kila kitu tofauti na hapa nchini. 

Spika amesema kuwa Rwanda wana Vyama vya ushindani, pasipo kutaja ni Chama gani cha upinzani anachokimaanisha kwa hapa Tanzania. 

"Tunaye mgeni kutoka Rwanda ni Spika wa Bunge lao anaitwa Donatile Mukabalisa,ni Spika kipindi cha 2, tofauti na hapa kwetu Spika wa Rwanda hatoki chama tawala,Rwanda hawana vyama vya Upinzani,hawana vyama vya kupinga kila kitu,wana vyama ushindani," alisema Spika akiwa anakaribisha wageni leo Bungeni jijini Dodoma. 

Spika wa Bunge la Rwanda Donatile Mukabalisa anatarajia kukaa nchini kwa siku tatu, katika ziara yake anatarajiwa kukutana na Wabunge, Kamati mbalimbali za Bunge, Chama cha Wabunge Wanawake (TGWP) , Pia atamtembelea Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje.

No comments

Powered by Blogger.