Viongoz 10 wa afrika kuhudhulia maziko ya mugabe




Viongozi 10 wa kiafrika wanatarajiwa kuhudhuria shughuli ya maziko ya rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Hayo yameelezwa na msemaji wa serikali leo katika wakati ambapo bado mvutano unaendelea juu ya wapi kiongozi huyo wa zamani anapaswa kuzikwa.

Mwili wa marehemu ulirudishwa Zimbabwe Jumatano ukitokea Singapore alikofariki akiwa na umri wa miaka 95.Miongoni mwa viongozi wa Afrika waliothibitisha kushiriki katika shughuli hiyo ni pamoja na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa,Uhuru Kenyatta wa Kenya,na Filipe Nyusi wa Msumbiji.

Marais wastaafu watakaoshiriki ni pamoja na Jacob Zuma wa Afrika Kusini,Kenneth Kaunda wa Zambia na Sam Nujoma wa Namibia.

Serikali ya Zimbabwe imesema Mugabe atazikwa Jumapili katika makaburi ya mashujaa wa kitaifa mjini Harare lakini familia ya kiongozi huyo wa zamani inataka kumzika karibu na kaburi la mamayake kama alivyotaka mwenyewe,katika kijiji cha Kutama,kiasi kilomita 85 kutoka mjini mkuu Harare.

Msemaji wa familia ya Mugabe pia amesema maziko yatafanyika wiki ijayo jumatatu au Jumanne.

No comments

Powered by Blogger.