Aina ya wachezaji wanaotakiwa na scouting wa nje
1)Mchezaji anae Control kwa mara moja na Control ya karibu sana wakati anapopewa mipira.(First Touch and close control)anapopokea mpira wowote.Yaani mpira usiende mita kadhaa nje ya miliki yako,(kwa Mujibu wa Wataalamu wa soka wa Vijana ni kuwa mara nyingi mchezaji mdogo anaposhindwa kuzuwia "Control" mpira mara moja,mara yake ya pili ya kutaka kuzuwia mpira huo huwa ni " tackle"ambapo ni uamuzi m'baya ambao utakuwa hauhitajiki katika ku Control mpira.
"Tackle" ipo katika sehemu yake nyingine isiyohusiana na ku Control mpira).
Kwa wachezaji wadogo kama hawakupewa mafunzo ya namna ya kumiliki mipira kwa mara moja na mengineyo huwapelekea wachezaji hao kukua na maamuzi yao kutoka udogoni hadi kufikia katika timu kubwa watakazochezea na hio ni mbaya zaidi kwa soka kwa vijana kwavile ndio msingi mzima wa soka kwa wakubwa na timu za Taifa za nchi.
2a)Mchezaji anaeamua kutoa pasi mara moja kwa haraka bila ya kuwa na matatizo "kigugumizi" katika maamuzi yake,yaani kuwa na utambuzi jinsi mpira unavyokuja na ataweza kutoa pasi mara moja kwa maamuzi gani ya haraka haraka.(Wataalamu wa soka wanakuwa na muda wanamuhesabia kila mchezaji mdogo katika maamuzi yake na kuangalia muda gani mchezaji mdogo "anaoganda" na mpira miguuni,"kwani kipindi mchezaji mdogo anapoganda na mpira huo,mpinzani anakuwa amefika pia kuuchukua mpira huo,hivyo humfanya mchezaji mdogo kuwa na matatizo ya maamuzi mazuri wakati ikitokea akimuona mpinzani chini ya mguu wake akichukua mpira huo").
Pengine anaweza kuwa mchezaji mzuri,ana control mzuri, lakini ana matatio ya kuwa na kigugumzi katika maamuzi yake kila anapopata mipira au kitu gani afanye katika kutoa pasi hio ,atoe kwa mchezaji gani?na aina gani ya pasi ambayo inaendana kwa wakati muafaka kwa mujimu wa mchezaji anaemkusudia yuko katika mazingira gani kumfikia pasi hio.(Kwa wachezaji wadogo wanatakiwa wataalamu wa soka kuweza kuwakuza na kutambua mafunzo na msingi wao wa kuwa wachezaji katika vilabu vikubwa pamoja na kuchezea timu za Taifa,vinginevyo ni hatari kubwa kwa Taifa kuwachia wachezaji wadogo wenyewe mitaani katika vilabu vidogo kujiendesha wenyewe bila wataalamu wa soka wa kuwaendeleza vijana hao ambao wengi wao wana vipaji vikubwa lakini vipaji vyao vinashindwa kufikia katika viwango vya kimataifa kulinganisha na vijana wa mataifa mengine kutokana na kukosa wataalamu wa kuwasaidia kuwajengea misingi mizuri).
b) Kwa mchezaji mdogo kama atafanya vinginevyo kutoa pasi za usumbufu kwa mchezaji mwenzake ni kupelekea kupoteza mipira ovyo au usumbufu kwa wachezaji wenzake kitu kinachosababisha kuigharimu timu nzima au mechi nzima kwa uzembe wa ukosefu wa utoaji wa pasi hizo zinavyotakiwa.
Kama mchezaji kijana ambae hatoweka karibu sana control yake anapopokea pasi ya aina yoyote kwa muda mwingi wa mchezo,pamoja na utoaji pasi zisizoona "hayo yanatokana na kila ambacho mchezaji huyo amejifunza tokea mwanzo wa msingi wake anapoanza kucheza soka,au upungufu wa utaalamu aliokuwa akiupata kutoka kwa walimu wake wakati akiwa katika hatua za mwanzo za kujifunza soka".
Mchezaji mdogo ambae ndie mchezaji mkubwa pia baadae kama akishindwa kufanya hayo hapo kutoweza kutokumiliki mpira vizuri au kutotoa pasi vizuri kwa mara moja kunapelekea sio tu usumbufu kwa mchezaji huyo bali pia kuharibu uwezekeano wa timu nzima kuharibu na kuchelewesha pia mfumo mzima wa uchezaji na pia kuchelewesha muda ambapo timu inakuwa na dakika 90 kuweza kuhakikisha kila mchezaji anatoa mchango mzuri katika dakika hizo.
(na kama itatokea mchezaji control yake na pasi zake kuwa pungufu kunachangia kupunguza uwezo wa timu kufanya vizuri,na kama kuna wachezaji zaidi ya mmoja katika timu hio ambao uwezo wao wa control na pasi ni mdogo basi kutapelekea timu yao kuwa na wakati mgumu kila mechi kwani dakika nyingi zitakuwa zinapotea kwa uzembe wa wachezaji kutokuwa na kutokuwa na control pamoja na uzembe wa kushindwa kutoa pasi za uhakika vitu ambavyo ndio msingi mkubwa kwa mchezaji yoyote timu hio au nchi hio itakumbana na wakati mgumu kila siku na wasitarajie miujiza katika soka,kwani unaweza kushinda mchezo mmoja kibahati lakini kila unaposhinda ndio unapoanza kuufata upinzani mkubwa huko mbele,ili kujijengea mazingira mazuri ya kukutana na vikwazo hivyo ni lazima ujijengee msingi mzuri kwa vijana wako ili waweze kukuwakilisha vizuri kila unaposonga mbele katika mashindano ya aina yoyote.
Scouting wengi wanaangalia sana kuhakikisha wanapata mchezaji ambae atakwenda kuongeza idadi tu katika timu,bali mchezaji ambae ana uwezo mkubwa katika hayo mambo muhimu kwa kila mchezaji kijana yakiwemo muhimu ya kwanza kabisa ni hayo hapo juu.
3)Mchezaji anaetumia akili zaidi kuliko nguvu katika mambo yake mengi anapokuwa hapo uwanjani,yaani akili inampelekea kumrahisishia mchezaji mdogo maamuzi haraka bila usumbufu kwa wataalamu au timu zitakazowachukua kwenda kufanyiwa majaribio ili kuweza kupata nafasi ya kujiunga na kuzichezea timu hizo.
4)Mchezaji anaeweka kichwa chake mbele.Yaani mchezaji anae angalia mbele na sio chini ya mguu wake.(hili ni suala kubwa sana ambalo wachezaji wengi kutoka barani africa na hasa kutoka nyumbani Tanzania wanashindwa kuwa nalo)
Pengine inaweza kuwa mchezaji ana uwezo mkubwa katika soka ,ana mambo mengi yanayohitajika,lakini vijana wengi wanashindwa kufungua vichwa vyao mbele na kuangalia mchezo mzima,yaani ni mchezaji gani ampatie pasi kwa wakati muafaka,kipindi mchezaji anapofanya vitendo vyake vya kumiliki mipira au kupiga chenga au kukimbia na mpira huku ukiangalia chini,ule muda ambao utanyanyua kichwa kutoa pasi au kufanya kitendo cha kufunga au hata kuokoa basi mambo mengi sana yanakuwa tayari yamebadilika kwa upande wa wapinzani na hata wachezaji wenzako,ambapo ukifungua kichwa na kuanza kumalizia kitendo chako hapo ndio inakuwa "labda"unatarajia katika ile ndoto ulipokuwa unaangalia chini hali itakuwa ndio ileile uliyoipanga wewe ukiwa unaangalia chini,lakini hali mara nyingi inakuwa sio hio hali inakuwa inabalika katika soka kila sekunde moja unapokuwa kiwanjani hivyo ni muhimu sana kwa wachezaji vijana kupatatiwa wataalamu wa soka katika timuzao ndogo kwani ndio hawahawa wachezaji ambao wanainamisha vichwa vyao katika timu zetu kubwa na timu zetu za Taifa.
5)Mchezaji anaejituma wakati wote kiwanjani,(kwa mujibu wa wataalamu mchezaji yeyote mzuri maisha hasimami kiwanjani,bali hujituma sana kila anapokuwa kiwanjani iwe mazoezi au mechi yoyote.
Mwisho wa somo letu la leo,kutokana na nchi yetu kutokuwa na wachezaji wanaochezea soka nje,ni vizuri tujijengea mazingira mazuri hapahapa nchini kwa kuanzisha Programe nzuri katika soka kwa vijana na kuhakikisha wanakuwa na matunzo pamoja na mafunzo katika kiwango cha kimataifa kwaajili ya taifa letu.
Hata kama tutakuwa hatuna wachezji wanaochezea soka nje katika timu zetu za taifa bali itakuwa wachezaji wetu wamejengeka katika misingi ya kimataifa sawa na wale wanaochezea nje.pia misingi hii ndio itakayopelekea Taifa kuuza wachezaji nje kwani watakuwa na uwezo sawa wale wa mataifa mengine ambao vijana wao hupata nafasi za kwenda nje na itapelekea vijana hao pia kuonekanwa nje pamoja na vilabu vikubwa nchini kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa vilevile vilabu vidogo kuwa vilabu vikubwa kwani kutakuwa na utajiri wa wachezaji vijana kila pembe hapa nchini.
habari hii imetoka kwa mmoja wa wataalamu na wapenzi wa O.F.A nchini Belgium.ambae alimalizia kwa kusema kutokana na usimamizi mzuri wa vijana nchini Ivory Coast ,karibu wachezaji wa timu yote ya taifa hilo wamepitia nchini Belgium kuanza Career zao lakini kabla ya hapo kule kwao wataalamu walikuwa wakiwafundisha ni jinsi gani mchezaji anatakiwa awe na vitu gani kuweza kujijengea msingi wa kucheza soka katika hadhi ya kimataifa hivyo wakipata nafasi inakuwa ni urahisi kwao kuweza kuzitumia vilivyo huku wachezaji wetu wakifeli katika majaribio kwani misingi yao huko chini ilikuwa ni kuangalia mpira chini na miguu yao wakiwa na mpira baada ya kuangalia juu kuzungusha kichwa kulia na kushoto na kuangalia mchezo unavyokwenda,
alimalizia kwa kusema wachezaji wengi nchini wanaanza kuchukuliwa na baadhi ya timu kubwa baada ya sasa hivi labda kuanzisha timu za vijana kwaajili ya timu zao kubwa kwa ajili ya hapo baadae kuzitumikia timu zao.na timu nyingine zilizobakia zinawachukua wachezaji vijana moja kwa moja katika timu zao kubwa kwa vile hawana timu za vijana ,
lakini cha msingi ni je wachezaji hao umri wao ni miaka 17 ,18 au 19 huo umri wao wote waliojifundisha soka huko chini ulikuwa ni msingi m'bovu usio na utaalamu,
unataka kum'balisha mchezaji katika umri wa miaka 18?
amejijengea mengi huko chini katika kuanzia kwake soka,hivyo kumuanzisha mchezaji umri huo kufungua kichwa juu akasoma mchezo itakuwa kama unamuulia uwezo wake katika soka,kwani itakuwa ukiangalia mbele kusoma mchezo wenyewe huku chini mpira atakuwa hauoni tena utampotea kwani atakuwa anashughulika na mambo mapya kabisa kinyume na mazowea yake yaliyopelekea wewe kumuona ni mchezaji bora,
lakini mchezaji huyo akikumbana na akina yaya touré,Keita,Essien,Obi Michel,ni lazima pale kati mchezaji wetu akishughulika kuangalia mpira na miguu yake chini na akija akiinua macho juu kutaka sasa kutoa pasi basi itakuwa hapo ni kuja kuanza mpira kati kuhesabu bao la wapinzani.
kuna bahati katika mchezo wa soka,lakini bahati hio haiji kila wakati na hasa kama hujajijengea mtazamo mzuri wa kuipata hio bahati kwa kucheza soka ya upinzani na kileo usitegemee kuipata bahati ya kuzifunga timu zote za wenzetu wa africa.Mashabiki wengi wengi wa soka Tanzania wanakiu ya kuziona timu zao zikifanya vizuri kimataifa.lakini tusitarajie na kuota bahati kwani vilabu vinazidi kuwa vikubwa barani Africa na timu za Africa hizi sasa zinatisha za taifa na wenzetu hawana woga tena hata wakicheza mechi dhidi ya taifa za ulaya au South America tunaziona jinsi wanavyotawala mchezo na kucheza "Solid"kabisa,tunahitajia tuzijenge timu za vijana wadogo kuwasaidia kuweza kutukomboa katika soka tusisubiri ndoto za kupata bahati kwani hatujakuwa tayari kuijenga na kuisubiri hio bahati pale kiwanjani.

Post a Comment