Serikali ya Rwanda yatoa chakula kwa walioathiriwa na amri ya kukaa nyumbani
Famalia zilizoathiriwa na sheria ya kukaa nyumbani , nchini Rwanda zimeanza kupokea msaada wa Chakula kutoka kwa serikali ya nchi hiyo.
Familia hizo ni zile zilizoathiriwa na agizo la kukaa nyumbani liliyowekwa nchini humo ili kukabiliana na maambukizi ya coronavirus.
Idadi ya visa vya maambukiziya coronavirus imefikia watu 60 huku wengine mamia kadhaa wakiendelea kuchunguzwa baada ya kukutana na visa vya awali.
Jumamosi pekee Rwanda ilitangaza visa 6 vipya vya coronavirus.
Hii inalifanya taifa la Rwanda kuwa na idadi kubwa zaidi ya visa vya virusi vya corona vilivyothibitishwa kuliko mataifa mengine ya Afrika Mashariki.
Hatua ya ugawaji wa chakula ilianza Jumamosi baada ya rais hiyo Paul Kagame kuelezea katika hotu#iba yake ya Jumamosi kuwa serikali yake itafanya kila kuwasaidia Wanyarwanda wanaoathiriwa zaidi katika kipndi cha agizo la kukaa nyumbani.
Bwana Kagame aliwaambia Wanyarwanda kuwa wategemee kuongezeka zaidi kwa visa vya coronavisus kadri watu wanaoshukiwa kuwa na visa hivyo wanavyoendelea kupimwa.
Wafanyakazi wanategemea malipo ya kila siku kwa ajili ya kuishi katika maeneo ya mijini ndio walioathiriwa zaidi kutokana na kusimamishwa kwa shughuli wanazozifanya.
Mpango wa ugawaji chakula umeanzia katika Mji Mkuu Kigali, lakini maafisa wanasema utaendelea katika miji mingine midogo nchini
Chakula kinachotolewa kimetoka katika hifadhi ya taifa vyakula vya nafaka unaosimamiwa na wizara ya na mifugo.
Mwanzoni mwa wiki hii, Rwanda ilitangaza kufunga mipaka yote ya nchi hiyo na watu kuamrishwa kusalia majumbani mwao katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
Hatua zingine zilizochukuliwa ni pamoja na watumishi wote wa serikali na wa kibinafsi kufanyia kazi nyumbani na safari za kuenda mikoani kusitishwa kwa wiki mbili kukiwa na uwezekano wa muda huo kuongezwa.
Vilabu vya pombe na, maduka yasio ya chakula pia yamefungwa huku usafiri wa bodabobda ukisitishwa.
Hatua hiyo ilichukuliwa siku moja baada ya wizara ya afya ya Rwanda siku ya Jumamosi kutangaza kuwa watu wengine sita wameambukizwa virusi vya corona miongoni mwao mtoto mchanga wa miezi 10.
Maambukizi hayo yanaifanya Rwanda kuwa na idadi ya visa 17 vya maambukizi ya virusi vya corona.
Kufungwa kwa shule zote za umma na za kibinafsi, maeneo ya kuabudu na sehemu zote za umma.

Post a Comment