Mfahamu Nguva kiundani zaidi

Nguva ni kiumbe ambaye amejizolea umaarufu mkubwa sana duniani, lakini umaarufu wake huo huishia kwenye jina tuu na si muonekano wake, kiuhalisia kiumbe huyu akionekana ni vigumu sana binadamu kumtambua kwamba ndiye nguva mwenyewe ambaye humzungumza nyakati tofauti, na yote hiyo ni kutokana na uvumi ambao umeenezwa ya kwamba eti nguva ni nusu mtu pia nusu samaki, tena samaki ambaye ni mwanamke, pamoja na uvumi huo lakini hata siku moja katika haikuwahi oneshwa viumbe hao madume wake hufanania vipi, pia haijawahi thibitishwa kwamba dume la nguva huyo avumaye naye huwa na muonekano huo huo wa samaki mwanamke. 

Ukweli juu ya nguva ni upi? 
Cha kwanza unachotakiwa kufahamu ni kwamba Nguva si samaki kama ivumishwavo, Kiumbe huyo ni mnyama aishiye majini kama alivyo kiboko tuu, kwa jina jingine huitwa Ng'ombe wa majini lakini kama utapenda majike yake huvuma kwa jina la malkia wa majini. 

Nguva ni miongoni mwa wanyama wenye bahati kubwa ya kuishi miaka mingi sana huzeeka akiwa na miaka 50 na huweza kugonga hata 70 na ushehe. Chakula chake kikuu ni majani, hupevuka wafikishapo miaka 9 mpaka 16 na mimba hubeba kwa miezi 13 mpaka 15, Nguva huzaa mtoto mmoja tuu, muda mfupi baada ya kuzaliwa mtoto hupelekwa juu ili apate nafasi ya kupata pumzi vyema na hunyonya kwa miezi 18 baada ya hapo hujifunza kutafuna majani na siku atapopevuka tuu biashara ya kukaa na mama yake huishia hapo. 

Kwanini nguva hufananishwa na samaki mwanamke? 
Nguva anafanishwa na umbile la mwanamke kwa sababu zifuatazo, mosi umbo lake harisi hufanania na nguruwe hivyo ili kumtengenezea picha nzuri isingelipendeza kama wangemvisha umbo lake hilo hilo na mchanganyiko wa binadamu, ndio maana wanasanaa huamua kumtengenezea kama samaki ingawaje mwili wake chini hauna miguu, ila juu ana mikono miwili yaani kulia na kushoto. 

Pili ana matiti mawili katika kifua chake kama ilivyo kwa mwanamke, tena yale yale yenye viwango vya ubichi ubichi (12:00 kamili pasina hata dakika mbele). 

Tatu ni mnyama mwenye aibu sana, hapendi kuonekana hovyo na wanadamu pengine labda ni kwa sababu ya 12:00 na isitoshe havai nguo, ufanano wa aibu yake ni sawa na binti anayeanza kupevuka halafu kwa bahati mbaya kifua chake kionekane hadharani walipojaa wanaume watupu waliomzidi umri. 

Nne ana malingo vilivyo pia ni fundi wa kudengua, kwa bahati mbaya mkagongana macho halafu afanye vitu vyake hivyo, kama ujasiri wako si wa mashaka unaweza kujitosa majini. 

Zifuatzo ndizo sifa za nguva; 

1. Hawana kasi katika kuzaliana na yote hii ni kwakuwa madume huwa mazoba katika mahaba. 

2. Nguva jike ndio huwa na tabia ya kubaini kuwa dume limepevuka hivyo majike ndio huyawinda madume, na hii hupelekea majike kutoka sana na madume yanayochipukia (sengereti hahaha) 

3. Watoto wa Nguva nao huitwa ndama. 

4. Katika jamii yao mapenzi si kitu cha wivu jike huweza kujipimia kiasi atakacho kwa madume tofauti tofauti.

5. Madume ya Nguva mapenzi kwao ni ziada sana, muda mwingi hujiweka bize kurinda mipaka yao tuu na shughuli nyingine mpaka hapo jike litapoamua kuwapigia misele. 

6. Ni wanyama ambao si wazuri sana katika kuogelea. 

7. Dume kwa kadri linavyozidi kuzeeka ndivyo ambavyo huzidi kupungukiwa nguvu za kiume. 

8. Jike huzaa kila baada ya miaka 3 mpaka 7. 

9. Ni wanyama wenye uzito mkubwa sana na wakubwa ni heri upewe kazi ya kubeba ng'ombe kuliko Nguva. 

10. Hula mimea inayomea majini na hutikisa kichwa chake baada ya kuweka chakula mdomoni kwa lengo la kutenganisha chakula na mchanga hususani pale atapoamua kutafuna na mizizi. 

11. Mkia wake upo katika muonekano wa bapa .

No comments

Powered by Blogger.