Simba Queens yaigaragaza vibaya Yanga Princess

Kikosi cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Yanga Princess katika mchezo wa Ligi ya Wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Women's Premier League uliochezwa Uwanja wa Karume. 

Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa ushindani mkubwa na ni kwa mara ya kwanza wanakutana kwenye mchezo huu kutokana na Yanga Princess kupanda msimu huu. 

Mabao ya Simba Queens yalifungwa Amina Ramadhani bao 1, Mwanahamis Omari mabao 4, Frola Kayanda mabao alijifunga 1 na Amina Ally 1. 

Simba Queens wanafikisha pointi 13 baada ya kucheza michezo mitano wakiwa nafasi ya pili huku Yanga Princess wakiwa nafasi ya saba baada ya kucheza michezo mitano wakiwa na pointi sita na kinara ni JKT Queens mwenye pointi 15.

No comments

Powered by Blogger.