FIFA yapendekeza wachezaji wa akiba 5 kubadilishwa katika kila mechi

Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, limependekeza leo kwamba timu ziruhusiwe kufanya mabadiliko ya wachezaji watano wanapocheza badala ya watatu kama suluhisho la muda.

 FIFA imesema pendekezo hilo litasaidia timu kukabiliana na shinikizo la kucheza mechi nyingi ili kukamilisha msimu kwa muda mfupi ambao umesalia, pindi mechi zitakaporejea tena baada ya kusitishwa kufuatia janga la COVID-19.

Pendekezo hilo litasubiri kuidhinishwa na baraza linaloshughulika na utungaji sheria za kandanda, IFAB, na uamuzi wa mwisho utatolewa na waandaaji wa michezo.

FIFA imesema hayo kupitia taarifa kwa njia ya barua pepe kwa shirika la habari la Reuters. Ligi mbalimbali za soka ulimwenguni zimesitishwa kwa sababu ya janga la corona.

Hata hivyo baadhi ya timu zimeanza kufanya mazoezi kujiandaa endapo mechi zitaruhusiwa kurejea tena.

No comments

Powered by Blogger.