Azam FC yakabwa koo na Ruvu Shooting

Timu ya Ruvu Shooting ya Pwani imetoa sare ya bila kufungana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. 

Kwa matokeo hayo Azam FC inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 18, ikiendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Yanga SC yenye pointi 53 za mechi 19 na mbele ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 33 za mechi 14. 

Ruvu Shooting inafikisha pointi 24 baada ya kucheza mechi 22 na kupanda kwa nafasi moja tu kutoka ya 14, sasa ikiwa mbele ya Stand United ya Shinyanga yenye pointi 23 za mechi 22. 

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mbao FC imeweza kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.  

Nayo Biashara United imeendelea kufanya vyema chini ya kocha mpya, Amri Said ‘Stam’ baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Stand United. 

African Lyon imepata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. 

Nayo Ndanda FC imeutumia vyema Uwanja wa nyumbani, Nangwanda Sijaona, Mtwara baada ya kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Tanzania 

No comments

Powered by Blogger.