Nay wa Mitego afunguka ishu ya ndoto ya Urais


Msanii wa Muziki, Nay wa Mitego amefunguka ishu ya kugombea nafasi ya uongozi  nchini. 

Nay wa Mitego ameiambia EATV, kuwa ana ndoto ya kuwa Rais wa nchi lakini Rais ambaye sio mwanasiasa. 

"Kwasababu sipendi siasa. Nina ndoto ya siku moja kuwa Rais wa nchi yangu lakini Rais ambaye sio mwanasiasa vitu vitakuwa vimenyooka hivi kama ninanyoosha vingine, " alisema Nay. 

Kipindi cha nyuma kulikuwa na tetesi kuwa Nay wa Mitego anataka kugombea Ubunge 2020 jambo ambalo Nay amekataa.

No comments

Powered by Blogger.