Simba wakwea pipa Leo kuwafata Mbabane FC


Kikosi cha Simba ambacho kitacheza mchezo wa marudiano na timu ya Mbabane Swalows FC ya Eswatini kimepaa leo kuwafuata wapinzani wake kikiwa na tahadhari ya kulinda heshima ambayo walijiwekea katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Simba walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-1 kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo wanatakiwa wasifungwe zaidi ya mabao 2 watakapocheza Desemba 4 kwenye mchezo wa marudio ili kusonga mbele. 

Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanatambua wanakwenda kucheza na timu bora na kubwa, kazi yao ni moja kuweza kupata matokeo mazuri. 

"Tunatambua tunakwenda kucheza na timu kubwa na bora, ila tuna kazi ya kulinda heshima yetu, tunajua sisi ni mabingwa wa Taifa na tunaliwakilisha, matokeo mabaya ni kujifedhehesha na kufuzu kwa Simba ni kujiweka sokoni kwa wachezaji kwenye rada za soka," alisema. 

Safari yao ya leo watapitia Johannseburg, Afrika Kusini kisha  watabadili ndege na kuelekea Manzini, Eswatini kwa ajili ya mchezo wao marudiano wa Ligi ya Mbaingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows. 

No comments

Powered by Blogger.