Kocha Yanga mpango wake huu


Baada ya kuilaza JKT Tanzania jumla ya mabao 3-0 katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kwa sasa mipango yake ni kuhakikisha Yanga haishuki kileleni.

Jeuri ya Zahera imekuja kufuatia timu hiyo kufika kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha jumla ya alama 35 nyuma ya Azam na Simba.

Mkongomani huyo ana imani timu yake itapambana kwa namna yoyote wanayoweza ili iweze kuendelea kushikilia usukani na ikiwezekana kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kauli ya Zahera inakuwa kama inaumiza wataniz zao wa jadi ambao wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 27 mpaka sasa.

Yanga baada ya kuifunga JKT ilifanikiwa kufikisha jumla ya mechi 13 iliyocheza na ikishinda mechi 11 huku ikisare mechi mbili pekee.

Wakati huohuo kikosi cha Yanga kesho Jumatatu kinashuka dimbani kucheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

No comments

Powered by Blogger.