Kikosi cha Simba chawasili Tanga

Kikosi cha klabu ya Simba kimewasili salama Tanga kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania. 

Kuelekea mechi hiyo itakayopigwa Jumamosi ya wikiendi ijayo, uongozi umesema hali na morali ya wachezaji ipo vizuri. 

Mabingwa hao watetezi wa ligi wanaenda kucheza na JKT wakiwa na alama 23 katika nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi. 

Wakati huo JKT ambao watakuwa nyumbani watapepetuana na Simba wakiwa na alama 18 kwenye msimamo wa ligi.

No comments

Powered by Blogger.