Michael Jackson aingiza US Dollar 400 Milioni kwa mwaka 2018, kivipi?

Kwa mwaka wa sita mfululizo Michael Jackson ameendelea kuikalia namba moja ya orodha ya watu maarufu waliofariki ambao wanaingiza pesa nyingi zaidi (Highest Paid Dead Celebrities) kwa mwaka huu 2018 amefanikiwa kuingiza kiasi cha $400 million sawa na zaidi ya Bilioni za 917 za Kitanzania tangu October 2017 hadi October 2018. 

Kiasi kikubwa cha mkwanja wake kimetokana na mauzo ya asilimia 50 za haki za kazi zake toka kampuni ya EMI Music Publishing kwenda Sony/TV ambapo asilimia 10 ilienda kwa familia yake. Mauzo mengine ya ziada toka kampuni yake ya Mijac Music Catalog. Pia haki za televisheni kwa kuruhusu kituo cha CBS kuonesha kipindi cha 'Michael Jackson Halloween' kwa mwaka wa pili mfululizo. 

No comments

Powered by Blogger.