Guardiola awapa tahadhari Real Madrid
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amewapa tahadhari Real Madrid kuwa ni ngumu kumpata kocha wa Tottenham Maurcio Pochettino huku akiushauri uongozi wa Spurs kuhakikisha unambakiza kocha huyo.
Akiongea kuelekea mchezo wa leo kati ya timu yake ya Man City dhidi ya Tottenham Pep amesema Pochettino ni kocha mzuri na klabu yake ya sasa inamuhitaji zaidi kuliko Real Madrid hivyo hadhani kama itakuwa rahisi kwa miamba hiyo ya soka barani Ulaya kumpata.
''Pochettino ameonesha uwezo Espanyol, Southmpton na sasa Tottenham unaweza kusema tayari ni kocha mkubwa na amekuwa akihusishwa mara nyingi na Real Madrid lakini sijui ni nini kinatokea nachowaza mimi sidhani kama ni rahisi kwa mmiliki Mr. Levy kumwachia'', amesema.
Kocha wa Real Madrid Julen Lopetegui yupo kwenye wakati mgumu hususani baada ya kipigo cha jana cha 5-1 kutoka kwa Barcelona, ambacho kimeifanya Real iwe kwenye nafasi ya 9 katika msimamo wa La Liga ikiwa na alama 14.
Ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa Rais wa Real Madrid Florentino Pérez ameripotiwa kuwa anataraji kujaribu kutuma maombi ya kumchukua kabla ya msimu huu kuisha.

Post a Comment