Matola ashindwa kumvumilia Malimi Busungu

Kocha wa Lipuli FC, Seleman Matola, amesema mshambuliaji wa timu yake Malimi Busungu amekuwa mtovu wa nidhamu na haeleweki wapi alipo baada ya kuondoka kambini bila taarifa. 

Katika kuelekea mchezo wa kesho kati ya timu yake dhidi ya Yanga, Matola ameeleza kuwa nyota huyo hayupo kikosini muda mrefu na hawajui yuko wapi na huo ni mwendelezo wa tabia zake zisizo za utovu wa nidhamu. 

''Busungu hayupo hata mimi sijui yuko wapi na nimeshatoa taarifa kwa uongozi. Lakini tabia za Malimi Busungu sio ngeni tangu yupo Yanga amekuwa hana nidhamu'', amesema Matola. 

Kuhusu mchezo wa kesho Matola amesema wamejipanga kupata ushindi kwani timu yao imepumzika vya kutosha baada ya kucheza na Mbao FC jijini Mwanza, hivyo wataingia uwanjani kesho kwaajili ya kusaka alama 3. 

Lipuli FC ipo katika nafasi ya 13 ikiwa na alama 12 kwenye mechi 10. Inaingia uwanjani ikiwa na ari kubwa baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

No comments

Powered by Blogger.