Mama na wanawe wanasurika kifo
Mama na watoto wake wawili wamenusurika kifo kwa baada ya kudondokewa na nyumba waliyokua wanaishi katika Kata ya Majengo, Manispaa ya kigoma Ujiji, mkoani Kigoma.
Akizungumza na Wandishi wa Habari, moja kati ya Mhanga wa ajali hiyo Site Hussen alisema chanzo cha ajali hiyo ni barabara iliyokua ikitengenezwa mtaani hapo na kusababisha nyumba nyingi mtaani hapo kuwa na nyufa.
“Ilikua Majira saa 7 usiku wa ndipo tulipo ndondokewa na nyumba mimi na watoto wangu wawili nilisikia kama nyumba inatikisika kisha undongo ukadondoka ikabidi niwahi kuangalia watoto wangu nilipofika chumbani ndipo ukuta wa nyumba ukatudondokea," alisema Hussen.
Kwa upande wake Mwanaharusi Hamisi Mkazi wa Mtaa wa Majengo alisema nyumba nyingi katika mtaa huo zimepata nyufa kutokana na ujenzi wa barabara, isitoshe msimu huu ni wamvua bado wana wasi wasi kuendelea kutokea kwa matukio mengine kama haya.
"Tunalalamika kulipwa fidia kwa madhara tuliyo yapata kutokana na ujenzi huu lakini hatujalipwa chochote hata kama ni kidogo tungepewa angalau tukaziba nyufa katika nyumba ili kuzuia madhara kama haya kujitokeza tena lakini tunaambiwa kuna marekebisho tulienda mwezi jana lakini tunajiuliza haya marekebisho mpaka lini,” alisema hamisi
Mganga mfawidhi wa zahanati ya Kigoma Uijji Ezie Mbwana amethibitisha kupokea majeruhi hao ambao ni mama na watoto wawili wote wa familia moja na kusema mtoto mmoja alipata majeraha kichwani hivyo jitihada zinaendelea kuwahudumia majeruhi hao na wanaendelea vizuri kwa sasa.
Post a Comment