Africa kwa kesi za corona zilizoripotiwa zapindukia 40,000
Hayo ni kwa mujibu wa takwimu mpya za Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) ambazo zinaonyesha kuwa, idadi ya vifo vilivyosababishwa na COVID-19 barani Afrika imefikia 1,689.
Kituo hicho kimesema kufikia jana Jumamosi kesi 40,746 za maambukizi ya virusi vya Corona zilikuwa zimethibitishwa barani Afrika, lakini habari njema ni kwamba wagonjwa zaidi ya 12,200 wa Corona wamepata afueni barani humo.
Hadi kufikia jana, idadi rasmi zilizokuwa zimetangazwa kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki; ni Tanzania wagonjwa 480, Kenya wagonjwa 435 na Uganda wagonjwa 88 wa corona. Walioaga dunia kwa Corona nchini Tanzania kufikia sasa ni watu 16 na Kenya ni watu 22.
Nchini Rwanda idadi ya watu walioambukizwa corona hadi sasa ni watu 243 huku idadi wa wagonjwa wa corona Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakifikia 674, kati ya hao, 33 wameshafariki dunia na 75 wengine wamesharejea katika hali nzuri za kiafya.
Virusi vya Corona vinaenea kwa kasi barani Afrika, na nchi zilizoathiriwa zaidi ni zile za kaskazini mwa bara hilo za Misri, Morocco, Algeria pamoja na Afrika Kusini.
Post a Comment