CORONA: Dunia yakumbwa na mgogoro wa njaa
Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limeonya kuwa, kufikia mwishoni mwa mwaka huu watu zaidi ya milioni 260 watakabiliwa na mgogoro mkubwa wa njaa kutokana na janga la Corona, hususan katika nchi za chini ya jangwa la Sahara barani Afrika.
Mkurugenzi Mkuu wa WFP, David Beasley amesema "katika senario mbaya zaidi, nchi zaidi ya 30 duniani zitakabiliwa na baa la njaa."
Amesema hatari kubwa inayojongea kwa kasi ni kuwa idadi kubwa ya watu watafariki dunia kutokana na taathira hasi za kiuchumi za mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 duniani hata kuliko Corona yenyewe.
Nayo Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Chakula (IFPRI) yenye makao makuu yake mjini Washington imetahadharisha kuwa, iwapo Pato Ghafi la Dunia (GDP) litapungua kwa asilimia 5 kutokana na janga la Corona, basi watu milioni 147 watatumbukia kwenye umaskini wa kupindukia.
Post a Comment