Vikwazo vya corona Ujerumani vitakuwepo hadi Aprili 20
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewashukuru Wajerumani na kusema kwamba kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakitekeleza hatua zilizotangazwa za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Huku idadi ya maambukizi nchini humo ikiwa inazidi kuongezeka, Mnadhimu mkuu wa ofisi ya kansela Helge Braun, amesema vizuizi hivyo havitaondolewa kabla ya tarehe 20, Aprili.
Kulingana na takwimu za jana za, Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza ya Robert Koch, watu 48,582 wamethibitihswa kupata maambukizi ya virusi hivyo nchini Ujerumani. Ni ongezeko la maambukizi ya watu 6,294 kutoka siku moja iliyopita.
Na idadi jumla ya vifo Ujerumani ni 325. Ujerumani imefunga shule, maduka, mikahawa, pamoja na viwanja vya michezo.
Na kampuni nyingi zimeacha kutengeneza bidhaa zake ili kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Post a Comment