Waziri Mkuu awapa kazi Wakuu wa Mikoa nchini
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Kilimo na Maafisa Biashara kote nchini wasimamie katika masoko yote na wajirishe iwapo vipimo vinavyotumika ni sahihi kwani lumbesa haikubaliki.
Ametoa agizo hilo wakati akijibu swali la Mbungewa Jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi aliyetaka kupata kauli ya Serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa katika kudhibiti unyonyaji wanaofanyiwa wakulima kupitia ufungaji wa mazao unaozidi viwango.
Waziri Mkuu amesema wanunuzi wa mazao mbalimbali lazima wafuate sharia, kanuni na taratibu za manunuzi ya mazao husika. “Maafisa Kilimo wasimamie biashara hiyo na waendeshe operesheni kwenye maeneo ya masoko ili kujirishana vipimo vinavyotumika.”
Amesema ni muhimu zaidi kutumia mizani ambayo haina utata ili kuwawezesha wakulima kuweza kunufaika kutokana na kilimo na kwamba suala la waununuzi kutumia vipimo visivyosahihi kama lumbesa halikubaliki.
Akijibuswali la Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa aliyetaka kupata kauli ya Serikali kuhusu kuhusu suala la ununuzi wa zao la pamba, Waziri Mkuu amesema Serikali imelifanyia kazi suala hilo na tayari zaidi ya tani 200,000 zimeshanunuliwa ambayo ni sawa na asilimia 80.
Waziri Mkuu amewahakikishia wakulima wa zao la pamba kwamba pamba yote iliyosailia majumbani itanunuliwa
Post a Comment