Halmashauri zatakiwa kuacha ubinafsi katika ardhi
Halmashauri nchini zimetakiwa kuacha tabia ya kufanya peke yake mambo yanayohusu ardhi kwakutozishirikisha taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa jamii.
Agizo hilo kwa halmashauri lilitolewa jana mjini Lindi na naibu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Angelina Mabula kwenye mkutano wa mashauriano baina ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara waliopo katika mkoa wa Lindi.
Waziri Mabula alisema halmashauri zinapopima miji na kutenga maeneo mbalimbali. Yakiwemo maeneo ya uwekezaji nilazima izishirikishe taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa jamii katika maeneo yanayopimwa na kutengwa. Kwani kutoshirikisha taasisi nyingine kunasababisha ziwe ni miongoni mwa sababu zinazosababisha migogoro.
Alisema miongoni mwa changamoto ni baadhi ya halmashauri kufanya mambo bila kushirikisha taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa jamii. Huku akiweka wazi kwamba maeneo ya uwekezaji na makazi yanapopimwa nilazima zishirikishe taasisi nyingine ili kuepuka migogoro.
Alisema upimaji sio kwaajili ya miji peke yake, bali hata vijiji. Kwani baadhi ya vijiji visivyopimwa vinapata wawekezaji. Hata hivyo kikwazo ni vijiji hivyo havjapimwa. Hali ambayo inasababisha migogoro au wawekezaji kushindwa kuwekeza katika vijiji hivyo.
Waziri Mabula amewataka wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa wilaya wasimamie kwaribu uandaaji mipango ya upimaji wa ardhi ili kuepuka migogoro ambayo inaweza kudhibitiwa.
Ameziagiza halmashauri zisimamie ulipaji kodi za ardhi. Huku akizitaka kuwa mfano kwa maeneo yanayomilikiwa na halmashauri yawe na hati. Kwani maeneo mengi yanayomilikiwa na halmashauri hayana hati.
"Rai yangu kwa wawekezaji, timizeni wajibu wenu wakulipa kodi ya ardhi. Halmashauri zisimamie ulipaji wa kodi hiyo," alisisitiza Mabula.
Post a Comment