Marekani mabingwa Kombe la Dunia Wanawake
Marekani imetwaa ubingwa wa Kombe la Dunia kwa Wanawake kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Uholanzi katika mchezo wa fainali uliopigwa leo kwenye Dimba la Lyon nchini Ufaransa.
Magoli ya Marekani kwenye mchezo huo yamefungwa na Megan Rapinoe dakika ya 61 pamoja na Rose Lavelle dakika ya 61.
Marekani walifikia hatua hiyo baada ya kuwatoa England kwa kipigo cha mabao 2-1 huku Uholanzi wakiwatoa Sweden kwa ushindi wa bao 1-0 kwenye michezo ya nusu fainali iliyopigwa Julai 2 na 3 mwaka huu.
Mshindi wa tatu katika fainali hizo ni Sweden ambaye alimfunga England mabao 2-1 kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu uliopigwa jana kwenye uwanja wa Allianz Riviera mjini Nice, Ufaransa.
Uholanzi walikuwa wakicheza fainali yao ya pili kwenye Kombe la Dunia huku Marekani wakicheza fainali ya tatu mfululizo.
Huu ni ubingwa wa nne kwa Marekani ikiwa pia imeshinda kombe hilo mwaka 1991, 1999 na 2015. Marekani wanachukua ubingwa huo wakiwa na kumbukumbu ya kipekee ya kuiadhibu Thailand kwa kipigo kikubwa zaidi kwenye fainali hizo cha mabao 13-0.
Post a Comment