Polisi Pwani wakusanya Tsh. Milioni 89.3 kutokana na makosa ya usalama barabarani
Jeshi la Polisi mkoani Pwani kupitia kikosi cha usalama barabarani limefanikiwa kukusanya zaidi ya Tsh. Milioni 89.3 kutokana na makosa ya usalama barabarani na madai ya serikali yapatayo 2,266.
Kupitia kikosi hicho lilifanya operesheni maalum yenye lengo la kudhibiti matumizi mabaya ya barabara ambapo walikamata makosa ya mwendokasi, kupita magari mengine sehemu isiyoruhusiwa na kupakia mizigo kupita kiasi.
Makosa mengine ni pamoja na madereva walevi na ukaguzi wa magari yanayobeba wanafunzi na pikipiki ambapo jumla ya makosa 1,680 yaliandikiwa faini na kukusanywa Tsh. Milioni 50.4.
Katika operesheni hiyo makosa ya magari na pikipiki yalikamatwa na watuhumiwa walionywa na wengine kutozwa faini ya papo kwa papo na magari yaliyokuwa na madai ya serikali kulipia madai.
Post a Comment