Haji wa Simba asema huu sio muda wa kuijadili Penalti ya Bocco

 

Mwenyekiti wa kipindi cha mpito wa tawi la Simba mkoa wa Manyara Haji Athumani amesema huu sio wakati wa kuendelea kujadili penalti iliyopigwa na nahodha wao John Raphael Bocco bali waendelee kuiombea timu ipate  ushindi jumamosi watakapovaana na TP Mazembe katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili wafanikiwe kutinga  hatua ya nusu fainali. 

Haji akizungumza na kituo cha redio cha Smile Fm mjini Babati amenukuliwa akisema Simba wana kila sababu ya kusonga mbele kwa kuwa wana uwezo mkubwa katika soka na kwamba watanzania wakiisapoti kama michezo iliyopita watapeperusha vyema Bendera ya Taifa. 

Kwa upande mwingine Haji amesema wamejipanga kuhakikisha wanawakusanya wapenzi na Mashabiki wa timu hiyo katika mkoa wa Manyara ili kuzidi kuimarisha nguvu na umoja wao,na kwamba kwa sasa wamefungua ofisi zao rasmi mjini Babati na wapo tayari kwa maoni na ushauri wakati wowote. 

Naye Rhoda Kimati mweka Hazina wa tawi la Simba mkoani Manyara amesema nia wanayo na uwezo wanao watahakikisha wanaungana kwa pamoja wana manyara hata kama ni kwenye runinga ili kuishuhudia timu yao ikifanya vizuri.

No comments

Powered by Blogger.