Sielewi Mabosi wangu wanakabiliwa na mashitaka gani - Shahidi


Meneja Rasilimaliwatu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mary Samson ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam namna vigogo watano wa shirika hilo wanaokabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka, walivyokuwa wakipanda vyeo. 

Amesema, haelewi mabosi wake wanakabiliwa na mashitaka gani. Miongoni mwa washitakiwa hao ni Mkurugenzi Mtendaji, James Mataragio. 

Akiongozwa na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Aneth Mavika, Samson amedai washitakiwa hao mpaka sasa bado ni watumishi wa TPDC. 

Amesema watuhumiwa walisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili. 

Alidai nyaraka za watumishi TPDC zipo katika majalada yanayotunzwa masijala ya siri na anawafahamu washitakiwa kwa kuwa ni watumishi wenzake, ni mabosi zake ila kwa sasa wamesimamishwa kazi. 

Amedai majalada ya washitakiwa hao kwa sasa yapo Takukuru na yalichukuliwa Januari mwaka huu ofisini kwao baada ya taasisi hiyo kuyahitaji kwa ajili ya uchunguzi. 

"Shirika lilipokea hati kutoka Takukuru iliyoelekeza kuhitaji majalada hayo agizo ambalo tulilitekeleza na tukayatoa Januari mwaka huu na tuliyakabidhi kwa barua" amedai Samson. 

Alidai jalada la mshitakiwa Mataragio linaonesha aliajiriwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Desemba 15, 2014, na alidumu katika nafasi hiyo hadi Agosti 24, 2016 aliposimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili. 

Alidai jalada la mshitakiwa George Seni linaonesha kuwa aliajiriwa TPDC Februari, 2014 na alitakiwa kuendelea na wadhifa aliokuwanao kutoka Ofisi za Bunge ambapo alikuwa Mhasibu Mkuu; hata hivyo alipofika TPDC hakukuwa na cheo hicho hivyo alipewa cheo cha Mkurugenzi wa Fedha

No comments

Powered by Blogger.