Serikali yawaasa Watanzania kuwasaidia watoto Yatima
Watanzania wameaswa kujitoa kwa kuwa hali na mali katika kuwasaidia watoto yatima wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto kwani wanayo mahitaji kama walivyo wengine wanaoishi majumbani na familia zao kwa kuwa kufanya hivyo ni kuugusa moyo wa Mungumoja kwa moja .
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenye ulemavu, Stella Ikupa, alipo tembelea na kutoa msaada katika Makao ya Watoto yatima Kurasini ,ambapo ametoa rai kwa watanzani kuendelea kujitoa wanapo pata nafasi kutembelea na kutoa misaada kwa watoto hao.
“Hawa ni watoto wetu tuendelee kujitoa tunakaamajumbani kwetu tunakula na kusaza tunamwaga vyakula kumbe kuna mtoto ambaye amelala njaa kwa sababu hana mzazi wa kumhudumia , kwahiyo nijambo jema tukitumia kidogo tunachokipata kugawana na wengine,hata Maandiko matakatifu yanasema, Dini iliyonjema ni kuwaona yatima na wajane katika shida zao na mtu anapofanya hivi anamgusa Mungu”Alisema
Aidha Ikupa ameushukuru uongozi ya Makao ya watoto hao kwa kuendelea kuwalea vizuri watoto hao na kuupongeza uongozi wa CCM kutoka Umoja wa wanawake (UWT) ambao nao waliambatana naye katika kutoa msaada huo pamoja na Mbunge wa viti maalumu Mariam Kisangi .
Kwa upande wake Afisa ustawi aliyemwakilisha Kamishina wa Ustawi wajamii ,Kutoka wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na wato,katika hafla hiyo Rehema Kombe ,amemshukuru mhe. Stella Ikupa, kwa moyo wake wa upendo na kuona umuhimu wa kuwasaidia na kutoa huma kwa yatima na kusema kuwa watohao ni watanzani kama walivyo wngine na wanamahitaji wanayo yahitaji na kutoa wito kwa viongozi wengine kuwa na myo huo .
“Wato hawa wamekosa wazazi wanahitaji ada za shule ,mavazi , chakula ,malazi na mengine yaliyo mahitaji ya kibinadamu , tunapo kwatuna sherehekea tunafurahi huko majumbani tuwakumbuke nawatoto hawa ,niwaombe sana viongozi , mashirika ,taasisi na watanzania kwa ujumla tuwajali niwatoto wetu sote kutoa nimyo ukitoa kidogo ulicho nacho Mungu anakubariki” Alisema
Wakitoa neno la shukrani watumishi na baadhi ya watoto, wameshukuru kwa kuwajali na kuwathamini pia wamesema wataendelea kumuombe kwa Mungu Mhe.Ikupa ili amuongezee palipo pungua na kumfungulia Baraka .
Mariam Kisangi ambaye ni Mbunge viti Maalumu Temeke , Mkoa wa Dar es salaam,akizungumza Makaoni hapo amewapongeza na kuwatiamoyo walezi na wafanyakazi wa kituo hicho na kuwaambia kuwa kazi wanayofanya ni kazi ya wito nikama kazi ya mungu na fungu lao kubwa liko kwa Mungu ,huku akipongeza serikali kwa maboresho ya kituo hicho kwani kipndi cha nyuma hakikuwa hivyo.
“Nawaomba watoto wetu mpendane na muwapende walezi wenu na walimu wenu ili muendelee na masomo”Alisema
Baadhi ya vitu vilivyo tolewa ni pamoja na ,mchele, Unga wa Ngano na sembe, ,Sabuni ya unga , miche,Matunda Madaftari kalamu,Sukari ,Mikate,Biscuits, Katoni za Juice,Mafuta ya kupikia na Taulo za kike.
Post a Comment