Mamlaka ya Mkemia Mkuu mbioni kuanzisha maabara ya vinasaba vya wanyama


Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kaskazini – Arusha,  ipo mbioni kuanzisha Maabara maalum Vinasaba vya wanyama ambayo itasaidia kutambua  asili ya mnyama ikiwemo wanyama waliopo ama waliokufa. 

Akizungumza wakati wa ziara maalum ya Maafisa Uhusiano waliotembelea Kanda hiyo leo, Meneja Kanda ya Kaskazini Christopher Anyango abainisha kuwa kwa sasa wapo katika ukarabati wa jengo ambalo Maabara hiyo itakuwepo. Awali ujenzi wa jengo hilo ulisimama baada ya ufadhili wake kukoma na hivyo kuilazimu Mamlaka  kufanya ukarabati ili kujipatia sehemu ya kufanyia kazi. 

“Maabara ya vinasaba vya wanyama ni muhimu sana. ukanda huu kutokana na kuwa na wanyama wengi na pia eneo la Kanda ya Kaskazini kuwa na watalii wengi ambao wanakuja kuona wanyama . Kwa sasa utaratibu unaendelea wa Kumalizia jengo hili na baadaye vitendea kazi kuwekwa ,“ameeleza Anyango. 

Anyango ameongeza kuwa suala la kuwatunza wanyama ili waendelee kuwepo, Ni suala la msingi na Maabara itakapokamilika hakuna sampuli zitakazosafirishwa nje ya  Kanda ya Kaskazini kwa uchunguzi. 

“Pale  hitaji litakapokuwapo kwa ajili ya uchunguzi wa wanyama hawa, baasi Kazi hii itafanyika hapa hapa Arusha.” Alisema Anyango.

Aidha, ametaja faida ambazo zitapatikana kwa Nchi ni pamoja na uwepo wa data zao kwa wanyama hao ikiwemo wanyama wanaolindwa Kimataifa kama Kifaru, tembo na wanyama wengine wengi ambao wapo hatarini kutoweka.

Maabara hii inatarajiwa kuwa ya kwanza Nchini na itakuwa ndio maabara Bora kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Maabara hiyo itaweza kufanya uchunguzi kwa wanyama wote wakiwemo walio hai na waliokufa.

No comments

Powered by Blogger.