DC Tabora aagiza mabadiliko kwa Watumishi soko kuu


Mkuu wa Wilaya ya Tabora,  Kitwala Komanya ameagiza mabadiliko ya watumishi wanaosimamia soko Kuu kwa lengo kuongeza ukusanyaji wa mapato katika soko hilo. 

Alisema baadhi yao ndio wamekuwa chanzo cha kuwafanya wafanyabiashara wakwepe ulipaji wa mapato na wengine wagome kulipa kwa sababu baadhi kuwa na maslahi ndani ya soko hilo. 

Komanya alisema hayo wakati wa  kikao maalumucha kupitia mapendekezo ya bajeti cha Kamati ya Ushauri Wilaya ya Tabora (DCC) cha Manispaa ya Tabora baada ya mjumbe mmoja kulalamika kuwepo na vitendo vinavyochangia upotevu wa mapato ya Serikali. 

Alisema kuwa wafanyakazi waliopo katika soko hilo hawatoshi kwa sababu haisaidii Manispaa kukusanya mapato bali wao ndio wamegeuka kama ni madalali wa wafanyabiashara hao na kusababisha ukusanyaji kidogo wa mapato. 

Kufuatia hali hiyo, Komanya alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji kuwaondoa mara moja na kuweka watumishi ambao ni wazalendo ambao watakuwa tayari kusimamia vema soko hilo kwa ajili ya maendeleo ya Manispaa ya Tabora na wakazi wake. 

Alisema hata alipotaka kukutana na wafanyabiashara wa soko hilo kujua kero zao ,watumishi hao walishindwa kumpa ushirikiano na kusababisha kutumia muda mwingi kusubiri iliapate mkutano wa wafanyabiashara hao. 

No comments

Powered by Blogger.