Kocha Patric Aussems: Sina mashaka na kikosi changu

Kocha wa klabu ya Simba, Patric Aussems amesema hana mashaka na uimara wa kikosi chake kimataifa kwani hesabu zake tayari zimekamilika kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya Congo. 

Simba leo walikuwa wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Boko kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa kimataifa dhidi ya AS Vita utakaochezwa Jumamosi nchini Congo. 

Aussems amesema wachezaji wake wana morali kubwa ya kushindana na ana imani ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao ujao. 

"Hakuna mashaka kwa wachezaji nimewapa mbinu mpya na tofauti kazi imebaki kwao kutimiza kile ambacho nimewaambia hasa wakiwa Uwanjani, ushindani ni mkubwa nasi tunapambana ili kufanya vizuri," alisema

No comments

Powered by Blogger.