Hii ndio sherehe kubwa kabisa nchini Afrika kusini kwaajili ya mwaka mpya ambayo hufanyika Januari 2

Mji wa Cape Town ambao ni maarufu kwa utalii nchini Afrika kusini umesherehekea mwaka mpya wa watumwa ujilikanao kama " Sherehe ya pili ya mwaka mpya". 

Cape Town inajulikana kutokana na nafasi muhimu iliyokuwa nayo wakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.Sherehe ya pili ya mwaka mpya iliandaliwa katika eneo lijulikanalo kama Distrix 6 la mji huo wa Cape town. Maelfu ya watu walihudhuria sherehe hizo. 

Darryl David, kiongozi wa Ken Fac Entertainer moja ya bendi zilizotumbuiza katika sherehe hizo alisema kwamba watumwa kutoka mashariki ya mbali walioletwa na wazungu waliokuwa wakiishi rasi ya Tumaini jema walikuwa wakifanya sherehe ya pili ya mwaka mpya kila Januari 2. Na wao kama wajukuu wa watu walioletwa kama watumwa katika rasi ya Tumaini jema wanauendeleza utamaduni huo. 

Waafrika kusini wenye asili ya kihindi na kimalay pamoja waafrika kusini weusi ambao ndio asilia wa eneo hilo kwa zaidi ya  miaka 150 wamekuwa wakisherekea sherehe hiyo ya mwaka mpya wa watumwa kila Januari 2. Sherehe hiyo ni moja ya sherehe kubwa kabisa nchini humo.

No comments

Powered by Blogger.