Mbosso kuachia wimbo na Diamond Platnumz siku ya wapendanao


Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Mbosso amesema kuwa ameshafanya wimbo na Diamond Platnumz ambao anatarajia kuutoa karibia na Valentine. 

Mbosso amesema kuwa Diamond alimwambia kuwa anapenda wimbo huo wa utoe karibia na Valentine. 

"Tayari nimefanya naye wimbo wangu mmoja, aliniambia mwenyewe anapenda tuutoe karibia na valentine kwahiyo kabla ya valentine watapokea zawadi kati yangu na Diamond,' alisema Mbosso. 

Ikumbukwe kuwa Mbosso hajawahi kutoa wimbo na msanii huyo wakiwa wawili zaidi ya kuwepo na msanii mwingine kama wimbo wa 'Jibebe' walioufanya na Lavalava. 

No comments

Powered by Blogger.