Ajinyonga kwa kuzuiwa mkesha
Mwaka Mpya wa 2019 umeanza na visa vya watu wawili wilayani Tarime mkoani Mara kufariki dunia kwa nyakati tofauti akiwemo msichana mkazi wa Mtaa wa Nkende, Elizabeth Magige (14) aliyejinyonga kwa kamba kwa madai ya kuzuiliwa na bibi yake kwenda kwenye sherehe za Mwaka Mpya.
Diwani wa Kata ya Nkende, Daniel Komote alisema."Tukio la msichana Elizabeth Mwita Magige wa miaka 14 kujinyonga nyumbani kwao lilitokea usiku wa kuamkia Januari mosi mwaka huu ambapo kulikuwa na sherehe za disko mjini Tarime ya kuamkia mkesha wa Mwaka Mpya na kuzuiliwa kwenda kuhudhuria mkesha huo. "Kitendo kilichomfanya binti huyo kushikwa na hasira na hatimaye kujitia kitanzi na mwili wake kukutwa asubuhi ukiwa unaning'inia ndani ya nyumba jirani na kwa bibi yake huyo aliyemkataza kwenda disko."
"Matukio ya watu kujinyonga katika Kata ya Nkende yamekuwa yakijitokeza viongozi wa dini, jamii ikiwemo familia zinatakiwa kuishi kwa amani na kumcha Mwenyezi Mungu huku vijana wakihimizwa kuacha kujichukulia maamuzi mabaya ya kujitoa uhai badala yake kusikiliza maneno ya wazee,"alisema Mwaibambe.
Mwili ya marehemu hao, ipo chumba cha maiti Hospitali ya Wilaya Tarime kwa uchunguzi zaidi kabla ya kuchukuliwa na ndugu zao kwa mazishi.
Post a Comment