Baada ya ushindi wa jana kwa Man United kuifunga Newcastle United 2-0, Ole Gunnar Solskjaer amefunguka na kusema kuwa hataki kuondoka klabuni hapo baada ya msimu huu kuisha. 

Solskjaer ameweza kurudisha morali kwa wachezaji wa Man United na kuingoza kupata ushindi katika mechi nne mfululizo. 

Pia amekua kocha wa kwanza kuweza kupata ushindi kwenye mechi nne za mwanzo katika klabu hiyo tangia Sir Matt Busby kufanya hivyo klabuni hapo.

No comments

Powered by Blogger.