26 wauawa katika shambulio Nigeria

Watu 26 waripotiwa kuuawa katishambulizi lilitekelezwa katika eneo la Sokoto Kaskazini-Magharibi mwa Nigeria. 

Gavana wa eneo hilo Aminu Waziri Tambawal ametoa taarifa kwa wanahabari kuwa  watu ambao hadi sasa bado hawajajulikana walishambulia maeneo tofauti  Sokoto na kusababisha vifo vya watu 26. 

Hayo Aminu Waziri Tambawal ameyasema akiwa katika shughuli ya mazishi na kulaani vikali wahalifu walioendesha  kitendo hicho cha kinyama. 

Taarifa zilizotolewa na  mashuhuda zinaarifu kwamba watu walioendesha shambulizi hilo walikuwa katika pikipiki 25. 

Jeshi la Nigeria limeweka doria  katika eneo hilo  baada ya shambulizi.

No comments

Powered by Blogger.