Mo Dewji unapigwa pesa na wapiga dili Simba - Afande Sele

 Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Afande Sele, ameshindwa kumkalia kimya beki mpya wa klabu ya Simba kutoka Ivory Coast anayeitwa Zana baada ya video inayomuonyesha akicheza mziki kusambaa mtandaoni. 

 Afande Sele kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika, "Yaani jitu linakwenda mpaka Afrika magharibi linatumia pesa kibao kisha linatuletea ushuzi huu pumbaff kabisa." 

"Mo pamoja na mapesa yake lakini kama ataendelea kuwaamini na kuwatumia wale wapiga dili wanaojiita makomandoo uchwara katika kutafuta wachezaji basi ajue kuwa ipo siku tutaletewa hata wacheza baikoko na kibao kata wa burkinafaso kisha tuambiwe ni mastriker hatari." 

"Alimalizia kwa kuandika, aliyelileta hili zigo pale Simba popote alipo ajifanye kama anajikuna maana kajua kutusukuma ndani daadek zake." 

No comments

Powered by Blogger.