Rais Magufuli amkabidhi kitita cha Milioni 10 rubani aliyetorosha ndege Kenya



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemkabidhi Sh.milioni 10 rubani mstaafu Nazizi Mapunda aliyetorosha ndege kutoka Kenya kuja Tanzania baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika. 

Rais Magufuli ametoa fedha hizo wakati wa kupokea ndege nyingine ya Air Bus 220-300 iliyowasili saa 10 jioni ikitokea jijini Accra, Ghana. 

"Waziri Kamwele amemtaja hapa Nahodha Mapunda, huyu ni mzalendo. Baada ya Shirika la Afrika Mashariki kuvunjika alikuwa Nairobi na waliambiwa wapaki ndege zote Nairobi, alijifanya kama anapaki lakini aliirusha na kuja nayo Tanzania" Rais Magufuli. 

Pamoja na kutoa fedha hizo, Rais Magufuli amelitaka Shirika la Ndege Tanzania, Kutomchaji fedha yoyote rubani huyo popote atakapo kuwa ana safiri yeye na mke wake siku zote za maisha yao.

No comments

Powered by Blogger.