Vanessa Mdee afunguka ishu ya kuwa na mtoto



Msanii wa Muziki, Vanessa Mdee amefunguka ishu ya kuwa na mtoto. 

Vanessa ameiambia Dizzim Online, amesema kuwa habari ya kuwa na mtoto ameisikia kwenye mitandao ya kijamii na ilimstaajabisha. 

"Hiyo ni habari ambao nimeisikia kwenye mitandao ya kijamii, yaani inanistaajabisha sijui hata nilimzaa lini huyo mtoto jamani mtu ameandika mtu ambaye nimezaa nae mtoto jamani nikasema kweli Watanzania tunajua sana kutunga stori huwa nachejaga sana nikisoma Comment," amesema Vanessa Mdee.

No comments

Powered by Blogger.