Fahamu vivutio vya utalii visiwani zanzibar

Na. Thabit Madai, Zanzibar. 
Watu wengi hawafahamu vivutio vilivyopo visiwa vya Zanzibar, ambapo huwa wanafikiria kuwa ina uzuri wa fukwe za bahari tu, La hasha, si fukwe tu bali kuna vivutio vingi vya asili ambavyo hupatikana ndani yake  nakuifanya kuwa maarufu zaidi  Duniani. 

Vivutio kama vile, mji mkongwe wa Zanzibar, Magofu ya kale, nyumba za ibada za zamani,utamaduni wa Mzanzibar, Kisiwa cha changuu, uwepo wa pomboo kizimkazi, maeneo yaliyokuwa wakiishi viongozi waliopita ambayo yana kumbu kumbu ya kutosha pamoja na Msitu wa Jozani. 



Hivyo ni baadhi ya tu ya vivutio vilivyopo ndani ya visiwa vya Zanzibar lakini makala hii leo itangalia kwa kina kivutio cha Msitu wa Jozani na neema za zilizosheheni ndani yake. 

Msitu wa Jozani 
Ni umbali wa kilometa 35 kutoka kusini mashariki mwa Unguja hadi kufika katika hifadhi ya msitu wa Jozani ambao hupatikana katika ghuba ya Chwaka, hifadhi hiyo imepakana na  vijiji tisa ambavyo ni Pete, kitogani, Ukongoroni, Chwaka,Unguja Ukuu,Charawe, Michamvi na cheju. 

Hifadhi ya  msitu  wa Jozani una vivutio vilivyogawika katika sehemu Tatu , vikiwemo Daraja la Mikoko, sehemu ya wanyama  pamoja na msitu. 

Daraja la Mikoko. 
Daraja la mikoko lipo kati moja ya kivutio ndani ya msitu huo kutokana na urefu wa daraja hilo pamoja na 

Miti ya Mikoko ilivyoshonana  na kunawiri vizuri katika maji chumvi yalioko chini ya Daraja hilo la mbao. 

Kwa umbali ni dakika 40 kwa miguu kuweza kulimaliza daraja hilo ambalo limepambwa na vipepeo aina mbali mbali kama vile Dadanesi na wengine wengi wenye rangi tofauti tofauti za kupendeza kama vile Karasisi ambaye hupatiakana Zanzibar tu. 

Mikoko hiyo ipo ya aina tatu : mikoko meupe,mikoko meusi na  mikoko mekundu(magando) ambayo ndio inaengeza hadhi ya Daraja hilo kutokana na miti hiyo kuwa na matawi mengi na mizizi yake huchomo juu ya ardhi kwa kiasi kikubwa jambao ambalo huwezi kuwamini kama mizizi waweza hisi nayo ni jumla ya matawi ya miti hiyo. 

Msitu 
Msitu huo una miti   ya aina mbali mbali kama mitondoo, mivinje , mikaratusi miti mafuta, mikonge, mikangara shamba na mingi mingineyo, ambayo ina urefu wa ajabu na kushonana juu yake jambo ambalo hufanya jua lisionekane katika eneo hilo. 

kuna baadhi ya miti ni dawa na hii mara nyingi hupatikana katika msitu huu wa Jozani kama vile Misiliza ambayo hutumika kama dawa ya kuondoa minyoo tumboni. 

Sehemu ya Wanyama 
Sehemu ya Wanyama ndani ya Msitu huo ndio iliyoibeba umarufu wa Msitu huo kwa kupatikana wanyama ambao adimukuonekana katika hifadhi nyingine yoyote Duniani. 

Wanyama hao kama vile vile  chura wa Jozani,Chuwi wa Zanzibar, Jongoo wa Jozani, Paa nunga na Kima punju (Red Colobus Monkey) ambao wamekuwa vivutio  vikubwa   vya  utali  na kuwafanya  watu kila kona ya Dunia kufunga safari na kwenda kuvingalia vivutio hivyo 

Katika Wanyama wote hao, Kimapunju ndio kivutio kikuu cha watalii kutokana na rangi yake ,umbile na tabia yao ya kuishi ujamaa kama Binadamu. 

kima Punje; 
Muonekana wa Kima Punju Uso wake ni mweusi una taji la manyoya meupe, rangi ya pinki kwenye midomo na pua na mkia mrefu wenye rangi nyeusi. 

Umri wa kuishi wa Kima Punju ni miaka 20 hivyo katika kipindi cha miaka  20 anayoishi duniani anaweza kuzaa watoto saba, ingawa anaweza kuzaa mapacha lakini huwa ni nadra kutokea. 

Kima mchanga anapozaliwa anakuwa mweusi lakini rangi yake hubadilika baada ya miezi sita. 

Kima Punju anabaleghe baada ya miaka 6 na anaeba ujauzito kwa miezi sita na kulea mtoto wake kwa miezi 16 kabla ya kupata mimba nyengine. 

Kima punju  huishi kwa kufuatana kwa makundi kwa wastani 50-80 kama wanavyoishi mbwa mwitu, na kila kundi la kima Punju  huwa kuna dume mmoja ambapo dume huyo kamwe hakubali kuliacha kundi hilo kuingiliwa na dume mwengine hadi kufa kwake. 

Ila Dume anaweza kupinduliwa nadume iwapo   mtoto wake amekuwa na na anataka kufaya mapinduzi aongoze yeye kundi, itambidi apigane na kiongozi wake ambaye ni baba yake. 

Kushinda katika mapigano hayo ndio paamfanya awe kiongozi wa knambapo ili mtoto afanye mapinduzi inamlazimu apigane na kiongozi wake ambaye huwa ni baba yake ili aongoze yeye kundi ashinde mapigano kwa kumjeruhi, kuumua au ampige hadi kukimbia. 

Inaelezwa kuwa Kima dume huonyonyeshwa zaidi kuliko jike, ananyonyeshwa ile aje kuwa na uwezo wa kuwa na familia yake, hivyo anakua akiwa na ndoto ya siku moja kuwa na familia yake hivyo anakuwa na nguvu zaidi kuliko jike. 

kila kundi linaishi mtaa wake na wanajuka kutoka mienendo yao ingawa mienendo yao hutofautiana kutoka na hali ya upatikanaji wa chakula. 

Kima punju hupendelea sana kula majani  machanga ya miti kama vilele vya mipera na majani ya mikungu ambayo ndio hupendelea kula zaidi jambo ambalo husababisha mikungu yote ya Jozani kutokuwa na majani kabisa kwani  yakichipua tu huliwa na wanyama hao. 

Chakula anachokula kima Punju hula maganda ya matunda  kama vile Embe, Mapera na makoroma ya nazi na hawali kabisa matunda yenye sukari  kama vile Embe mbivu ,Ndizi mbivu  kutokana na matumbo yao kushindwa kusaga vitu vya sukari (insuline  hormone) hali hii huwafanya kutokuwa na uhasama na kima wengine. 

Vile vile Kima punju hupendelea kula makaa  meusi kama tiba ya maradhi mbali mbali yanayowasumbua na ni kinga  ya maradhi yao. 

Cha Ajabu ambacho anacho kima punju huwa nacho kuwa  hukaa  zaidi ya miezi mitano bila kunywa maji kutokana na vyakula wanavyokula si kumtaka kunywa maji, kwani mara nyingi hula vyakula vyenye ukakasi vikiwemo vya  majani machanga. 

Kikawaida Kima punju huwa wanaishi  maisha ya kupendana wao  wenyewe kwa wenyewe  pia huwa  hupenda sana kuwatizama watu wanafika katika eneo lao  kwa lengo kuwangalia wao, Mara nyingi hufurahi na kucheza wakiwa na watu kama vile watalii katika eneo lao. 

Furaha yao inamaanisha kuwa ni Faraja ya moyoni kwa kutembelea, Tabia hii huwa nayo kima tu pekee ambapo binadamu unapo waita huwa wanakua na kucheza pamoja lakini kitu ambacho huchukia zaidi ni kupigwa. 

Wageni wengi wakifika eneo lao kima punju huwa wanashuka na kuwapokea wageni hao huku wakiwa wenye lengo la kupokea zawadi mulizowaletea kama vile ndizi n.k. 

Kuna Tabia ambayo kima Punju huwa nayo kama alivyotueleza Mkuu wa Hifadhi ya msitu Khamis Moh’d alisema kuwa Kima punju huwa anatabia ya kuwakimbia watu wenye Asili ya watu weusi( afrikan people) 

“hii inatokana kuwa hapo awali wakazi wa vijiji vinavyozunguka na hifadhii walikuwa wakiwapiga mawe kutokana na kuwalia mazao ya mashambani pia kuvamia makazi wanayoishi binadamu” alisema Khamis Moh”d ambae ni mkuu wa hifadhi  ya msitu wa  Jozani. 

Mradi wa kuhifadhi msitu wa Jozani wa Jozani-Chwaka Bay Conservation Project uliokuwepo kati ya mwaka 1995 mpaka mwaka 2003 ulimchagua mnyama huyu kuwa kwenye nembo ya utunzaji mazingira Zanzibar. 

Yote kwa yote cha kusikitisha kuwa Kima punju wako kwenye hatari kubwa ya kupotea ambapo  tayari Shirika la Kuhufadhi Wanyamapori Duniani (IUCN) limewaweka kwenye mstari mwekundu. Hali hii imetokana na makazi hao kuharibiwa na binadamu kwa uvunaji wa miti kwa ajili ya mbao, uchomaji wa misitu na usafishaji wa misitu kwa ajili ya mashamba. 

Ambapo Kwa sasa idadi yao imepungua hadi kufikia chini ya 3,000 kutokana na uharibifu wa msitu kunakosababisha kupungua eneo lao la kutafuta malisho na kupelekea kupigana wao kwa wao. 

Faida ya hifadhi ya Jozani. 
Mkuu wa kitengo cha Utalii  Salum Ramadhani alisema kuwa Msitu wa Jozani ni miongoni mwa sekta muhimu ya utalii yenye kuingiza fedha nyingi  kwa serikali,kutokana na kuwa na vivutio vya kila namna katika hifadhi hiyo. 

“Kila mwaka tunapokea  wageni kutoka  sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi takribani 25,000 kwa mwaka  ambao huchangia  zaidi ya Tsh milioni 400,” alifafanua ndugu Salum Ramadhani. 

 “Aidha alisema    wageni wengi kutoka nchi za Ujerumani, Uingereza, Marekani,Ufaransa na Italia,    Wageni wengi zaidi hutoka utaliana   kutokana na kuwa na usafiri wa moja kwa moja,”  aliendelea  kueleza ndugu Salum. 

Aliendelea kwa kusema kuwa mapato yanayopatikana  kutokana na uingiaji wa wageni hao hugawa  katika mafungu mawili alifahamisha kuwa,Fungu la kwanza ni la serikali ambalo ni asilimia 50 na fungu la pili ni la wanavijiji ambalo nalo ni asilimia 50  kwa  wanavijiji waliozunguuka hifadhi hiyo. 

“  Hii ni    Kutokana na kuharibiwa  mazao yao  na wanyama waharibifu kama kima,Nguruwe pamoja na wanyama wengine na kukosa maeneo ya kutosha kwa  ajili ya  kilimo  kikiwemo kijiji cha Pete kutokana na eneo kubwa la ardhi  yao kuingia ndani ya hifadhi hiyo,”  alifafanua ndugu Salum.1/29/2015 

 Nae mmoja  miongoni mwa wanavijiji hao Moh’d Ali Mchobwa alisema kuwa  kwa sasa wanafaidika na hifadhi  hiyo kwa kupokea fedha kutoka  katika mgao wa kila mwaka na kufanikiwa kujenga skuli kwa maendeleo ya watoto wao. 

“Zamani walikuwa watoto wanapata tabu sana maana wanatembea masafa marefu kufuata Elimu kwenye vijiji vya mbali kama vile Kitogani na Muyuni” .alisema ndugu Mchobwa. 

Hata hivyo ,mkuu wa hifadhi hiyo alisema, licha ya Hifadhi hiyo kuwa na faida nyingi pia hukabilwa na changamoto mbali mbali zikiwemo kuungua moto   kila baada ya mwaka   kutokana na mkusanyiko wa majani mengi  ambayo  hupelekea kuwaka moto wenyewe. 

Aidha sababu nyengine zinazopelekea   msitu huo kuungua moto  ni uvunaji haramu wa Asali pamoja na wasasi ambao hutafuta wanyama   kama nguruwe na Paa kwa ajili ya  kitoweo,Hivyo kutokana na kazi hiyo ngumu ya uwindaji ambayo hufanywa wakati wa usiku  baadhi ya wasasi huvuta sigara na vipande hutupwa na kusababisha mlipuko wa moto. 

 Pia aliendelea kwa kusema  kuwa wanao  walinzi mbali mbali lakini bado suala hilo linakuwa guumu kutokana na ukubwa wa  Hifadhi hiyo. 

Alisema  kutokea kwa moto husababisha  kukimbia kwa wanyama kama vile paa  na hata wanyama wengine ambao ni wazito kukimbia hufa  mfano Chatu, Nyoka na hata wadudu wadogo wadogo wakiwemo Jongoo wa Jozani pamoja na miti ya asili kutoweka. 

Hifadhi ya Jozani si hifadhi ya  kuoteshwa bali ya asili  na rasilimali zilizomo zimehifadhiwa tangu zamani. 

Katika eneo la Jozani palikuwa na mtawala aliyejulikana kwa jina la JOSHI, ambae alikuwa mfanya biashara wa kihindi.Mfanya biashara huyo  alikuw 

a akiishi eneo hilo mnamo mwaka 1930 hadi kufikia 1996 msitu huu ulirejeshwa mikononi mwa wanavijiji ilikuwa ni hatua ya kwanza kuhifadhi na kuulinda. 

Mfanya biashara huyo ambae alikuwa akiishi karibu na Bwawa la Mwajoza   ambalo alikuwa akitumia kwa shughuli  mbali mbali za kila siku, Hivyo  jina la  mtawala Joshi  na eneo alilokuwa akiishi Mwajoza ikapelekea kupatikana kwa jina la Jozani.

No comments

Powered by Blogger.