Ujumbe wa manung’uniko, kilio kusomwa makanisani

LEO ni Sikukuu ya Krismasi ambapo waumini Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) zaidi Mil 6.5 wanatarajia kusomewa waraka huo uliobeba manung’uniko, majonzi kulingana na hali ilivyo kwa sasa. Anaripoti Regina Mkonde … 

Waraka huo uliotolewa na Mkuu wa KKKT, Askofu Frederick Shoo utasomwa leo kwenye makanisa hayo ukijikita katika kuishauri serikali kusimamia haki ili hupunguza manung’uniko kwa Wananchi. 

Ujumbe huo unaonesha namna wananchi wanavyopoteza matumaini huku wakijaa manung’uniko kutokana na hali zao za maisha. 

Umeeleza namna jamii inavyopita kwenye changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na vitendo vya ubakaji, ukeketaji pia ndoa za utoni na kila aina ya mateso. 

Dk. Shoo ameeleza kuwa, matatizo mengine yanatokana na umasikini wa Wananchi unaosababisha kuibuka kwa manung’uniko na hofu katika maisha ya Watanzania hivyo kuoelekea kukosa matumaini. 

No comments

Powered by Blogger.