Makala: Navy Kenzo na Diamond 'waikosa rekodi' ya Harmonize

Kundi la muziki Bongo, Navy Kenzo bado linaendelea kufanya vizuri na wimbo wao mpya 'Katika' ambao Wamemshirikisha Diamond Platnumz. 

Taarifa nzuri ni kwamba wimbo huo uliotoka September 27, 2018 umeweza kufikisha views milioni 5 kwenye mtandao wa YouTube. 

Hivyo kwa sasa wimbo Katika unafukuzia rekodi ya wimbo wao Kamatia ambao walitoka miaka miwili iliyopita. 

Nyimbo za Navy Kenzo zilizofanikiwa kufikisha views zaidi ya Milioni 2 ni kama Feel Good ambao wamemshirikisha Wildad, pia kuna Game ambao walifanya na Vanessa Mdee. 

Kwanini Harmonize  

Tunarudi nyuma hadi April 14, 2018 ambapo Harmonize alitoa wimbo wake Kwangwaru ambao alimshirikisha Diamond Platnumz. 

Wimbo huo ulifikisha views milioni 10 katika mtandao wa YouTube kwa kipindi cha mwezi mmoja na kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kufanya hivyo. Hadi sasa wimbo huo umefikisha views zaidi Milioni 30 na kuwa wimbo wa kwanza wa msanii huo kufanya hivyo. 


Kumbukumbu Muhimu  

Tanzania kwa sasa kuna video tatu tu za muziki zilizofikisha views zaidi ya Milioni 30 kwenye mtandao wa YouTube. Video hizo ni Nana na My Number Remix za Diamond Platnumz, pamoja na ile ya Harmonize Kwangwaru. 

Wimbo uliotazama zaidi Tanzania pia ni wa Diamond 'Nana' ambao amemshirikisha Mr. Flavour kutoka nchini Nigeria. Wimbo huo ulitoka  May 29, 2015 na video yake iliongozwa na Godfather nchini Afrika Kusini. 

No comments

Powered by Blogger.