Bunge kuanza kuunguruma kesho




Mkutano wa 13 wa Bunge la 11 utaanza kesho Novemba 5,2018, huku miswada ya sheria mitano ikitarajiwa kusomwa ukiwemo wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2018.

Spika wa Bunge, Job Ndugai  leo amesema miswada mingine ni wa maji na usafi wa mazingira, marekebisho ya sheria mbalimbali namba nne wa mwaka 2018, muswada wa mamlaka ya hali ya hewa wa mwaka 2018 na wa mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu.

" Kupitia kwenu naomba tuwafahamishe Watanzania kuwa kesho ni siku yetu rasmi tutakayo anza vikao vyetu vya ndani ya ukumbi wa Bunge vya Mkutano wetu wa 13 kwa Bunge hili la 11 ambalo mimi ndio Spika wake," alisema Spika Ndugai. 

Aidha Spika alisema Shughuli ya kwanza kufanyika katika Bunge hilo ni kuapishwa kwa Wabunge wanne ambao ni Thimotheo Mzava (Korogwe Vijijini), Mwita Waitara (Ukonga), Julius Kalanga (Monduli) na Zuberi Kuchauka (Liwale)ambao wote ni Wabunge wa CCM.

Ndugai aliongeza kuwa, maswali 125 yakawaida yataulizwa na waheshimiwa Wabunge na maswali 16  yataulizwa kwa Waziri Mkuu.

No comments

Powered by Blogger.