Asali ni chaguo la kwanza kutibu kikohozi


Asali yatajwa kuwa ni chaguo la kwanza kuliko dawa nyengine za matibabu ya kikohozi, mwongozo mpya wa kitabibu umependekeza. 

Madaktari wanatakiwa kutoa kwa uchache sana dawa za kuua vijidudu maarufu kama antiBiotic kwa sababu katika kesi mbali mbali imebainika kuwa zinafanya kazi ndogo sana katika kupunguza kikohozi, maafisa wa afya wanasema. 

Mara nyingi kikohozi hupungua chenyewe ndani ya wiki mbili mpaka tatu. 

Mapendekezo hayo mapya kwa madaktari yanalenga kupunguza tatizo la dawa za antibiotic kugoma kufanya kazi. 

Kutumia sana dawa za antibiotiki kunafanya kuwepo na ugumu katika kutibu maambukizi, kwani hutengeneza uzio unao zuia dawa hizo kufanya kazi. 

Kinywaji cha moto chenye asali na maranyingi kikiongezewa limao na tangawizi ni kinywaji maarufu cha kutibu kikohozi na mafua lakini pia kinyaji hiki hutengenezwa nyumbani. 

Mapendekezo mapya kutoka katika taasisi ya kitaifa ya afya na huduma bora (NICE) na afya ya umma Uingereza (PHE) wanasema kuna ushahidi mdogo kwamba inaweza kuwasaidia kuboresha dalili ya kikohozi. 

Dawa za kikohozi zilizo beba pelargonium, guaifenesin au dextromethorphan zinaweza pia kuwa na manufaa, wanasema. 

Wagonjwa wanashauriwa kutumia tiba hizo na kusubiri dalili kuondoka zenyewe kabla ya kuanza kutumia antibiotic. 

Mara nyingi kikohozi husababishwa na vijidudu ambavyo haviwezi kutibiwa na dawa za antibiotic lakini huondoka vyenyewe. 

Lakini pamoja na kutambua ukweli huo tafiti zinaonyesha asilimia 48 ya madaktari wa kawaida wanatoa dawa za antibiotic kwaajili ya kutibu kikohozi au homa ya kooho. 

Dkt Tessa Lewis, ambaye ni mwenyekiti wa kikundi cha watoa mwongozo wa kutoa dawa kitabibu amesema, "iwapo kikohozi kitazidi badala ya kupoa, ama mgonjwa akaendelea kujisikia vibaya na kushindwa kuhema basi mgonjwa itambidi amuone daktari." 

Rasimu ya mapendekezo hayo ni sehemu ya mapendekezo mapya ya kanuni za utoaji wa dawa za kuua vijidudu ambazo zinaandaliwa kwa pamoja na PHE na NICE. 

Daktari Mkuu wa Uingereza Profesa Dame Sally Davies, awali alishaonya juu ya usugu wa matumizi ya dawa za kuua vijidudu. Pale dawa hizo zinaposhindwa kufanya kazi, maambukizi yanakuwa magumu kutibika, pia njia za kawaida za kimatibabu kwa magonjwa kama saratani na kupandikiza viungo zinakuwa hatari kufanyika, ametahadharisha Profesa Davies. 

No comments

Powered by Blogger.